IBADA IN THE CITY MBEYA


Muimbaji wa nyimbo za injili Dr Ipyana Peter Kibona ameandaa Ibada nyingine jijini Mbeya hii ni baada ya kuandaa Ibada In The City Jijini Mwanza sasa hivi ameamua kuhamishia Ibada hii nyumbani kwao mjini mbeya ambapo amesema huduma hii itakuwa inafanyika kwa kanda Ibada In The City imelenga katika kumfanyia Mungu Ibada na kufanya watu wa kila rika na kabila zote wakutane na Mungu kupitia Ibada hii ,Pia Dr ameweka wazi pia siku hiyo nyimbo zake zote zilizobebwa kwenye Album inayofahamika kwa jina la MOYO WANGU ibada TWENTY18 ambayo imefanyiwa Mixing mjini Prectoria South Africa ataimba Live akishirikiana na wapakwa Mafuta wengine . Akiongezea amesema pia kwa vijana wote wa vyuoni vilivyo mjini Mbeya hapa akizungumzia  Mzumbe,Must,Sauti,Teku,Udsm,Utumishi,Grace college na wengine wote kuwa wafike kwa wingi kwani Mungu kuna kitu ameandaa kwa ajili yao  Ibada hiyo inayotegemewa kufanyika ,mnamo  Tarehe 17 ya mwezi November mwaka huu  katika ukumbi Mkubwa unaofahamika kama Tughimbe Hall unaopatikana Mwanjelwa pamoja na hayo Dr Ameweka wazi kuwa atakua na muda mnzuri kufanya Ibada na baadhi ya fellowship za vyuo mbalimbali kutokana na ratiba zitakavyokuwa hii ni kabla ya siku ya Ibada in The City ambapo tarehe rasmi haijawa rasmi
Mwishoni amemalizia kwa kusema [IbadaMalangoniMbeya][IbadaInTheCityMbeya]

Post a Comment

0 Comments