EPISODE YA 2 PADRI MLA NYAMA ZA WATU


Nikakumbuka kuwa, wakati wanaingia, walipitia njia zote za uumini, na pia walionekana ni wanyenyekevu kupita hata waumini wangu wa kila siku.
Wakati nikiwaza hayo, ghafla mmoja wa wale wazee alisimama mbele yangu bila kumwona akitoka kwenye fomu kuja mbele, nikashituka, lakini kumbe waumini wengine waliniona nilivyoshituka, wakakaza macho kiwangu wakishangaa.
Nilikatisha maneno ya ibada na kuinua mikono juu kisha nikafanya ishara ya msalaba, kwa jina la baba, la mwana na la roho.
Akapotea mbele ya macho yangu na kuonekana amekaa na mwezake kama mwanzoni, wakacheka sana lakini si kwa kutoa sauti.
"Nilishtuka sana, nikafikicha macho kuyaweka sawasawa kwani yalionekana kama yana ukungu wa moshi.
Yalipokaa sawasawa, nikaendelea na ibada lakini mwili wangu ukiwa umechoka sana, hauna nguvu tena mwilini kama kuna vitu vunatembeatembea.
Baadhi ya waumini walipata picha hiyo, kwamba sikuwa sawasawa, lakini walikuwa hawajui kama nilikuwa naona watu wa ajabu.
Nilipofika eneo la kuongea maneno ambayo ikawalazimu waumini wasimame, wale wazee wawili wakawa wa kwanza kusimama kabla sijamaliza maneno na wakawa warefu kuliko waumini wangine.
Kurefuka kwao kama kuliambatana na moshi mkubwa wa moto wa kuni.
Nilipowaangalia waumini wengine walionekana hakuna wanalolijua kuhusu maono yangu kwani walisimama, wakafunga mikono kwa unyenyekevu mkubwa wakinisikiliza.
Kama wangekuwa wamegundua kitu, basi hata wale waumini waliokaa jirani wangejua, kwani wao walikuwa wakinitazama tu wakati jirani yao kuna mambo ya ajabu!
Nilikata maneno ya ibada na kuwaamuru waumini wakae, wakatii lakini mshangao:
"Humu ndani kuna watu wawili naona kama si wa imani yetu," nilisema.
Waumini wote wakawa wanageukageuka na kutazamana wakiwatafuta hao watu wawili.
Walichokifanya wale wazee sasa, muumini aliyekaa katikati yao alipogeuka kumwangalia mmoja wao, wakaonekana wote wamekaa pamoja na yule muumini akawa amekaa pembeni yao, kwa hiyo alipogeuka akawa anamwangalia muumini ambaye anamfahamu.
"Naamini hakuna atakayeweza kuwaona, maana wanatumika sana na ibilisi," nilisema.
Ninawapa muda wa wao kujisema ni akina nani?" Nilisema huku nikiwaangalia kwa kuwakazia macho huku waumini nao wakinikazia macho mimi na kuyafuatilia ninakoangalia.
Je nini kitaendelea usikose kufatilia sehemu Ya tatu hapa hapa mzumbesokoni.blogspot.com

Post a Comment

0 Comments