Asilimia kubwa ya watu hupiga simu na kutumia Internet pamoja na kutuma SMS kwa kutumia salio la kawaida, yote hiyo ni sababu ya ujio wa vifurushi ambavyo watu wengi hutumia ili kubana matumizi na kuepukana na gharama zisizokuwa na ulazima.
Lakini kadri siku zinavyo zidi kwenda gharama za vifurushi hivi zinazidi kupanda kwa kasi na hii kusababisha matumizi ya simu kuwa magumu na kupelekea wateja wa mitandao kuhama hama kila mara. Sasa kuliona hilo leo Tanzania Tech tumekuletea aina mbalimbali za vifurushi vya bei nafuu ikiwa pamoja na njia za kuweza kujiunga na vifurushi hivyo.
Vifurushi hivyo vimejipanga kulingana na mtandao hivyo hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu kila siku kwani tutakuwa tukiweka aina mpya za vifurushi pindi tutakapo kuwa tumevipata, basi bila kupoteza wakati basi twende tukangalie vifurushi hivi.
YALIYOMO:
Vodacom Tanzania
Tigo Tanzania (University offers *148*01*20# then 3)
TTCL Tanzania
Halotel Tanzania
Airtel Tanzania
Vodacom Tanzania
Kama wewe upo Dar es salaam basi unaweza kufaidi kifurushi cha DAR SUPA UNI kwani kifurushi hichi ni cha gharama nafuu sana. Kifurushi hichi kinakupa.
MUDA – Masaa 24 (Kwa Siku)
Voda kwenda Voda – Dakika 30
Mitandao Yote – Dakika 20
SMS – 500
Internet – MB500
Bei – Tsh 500
MUDA – Masaa 24 (Kwa Siku)
Mitandao Yote – Dakika 55
SMS – 50
Internet – Haina Internet
Bei – Tsh 1000
MUDA – Siku 7
Voda kwenda Voda – Dakika 150
Mitandao Yote – Dakika 50
SMS – 2000
Internet – GB 1
Bei – Tsh 2000
Vifurushi hivi vingi vinakuja na WhatsApp, Facebook na Instagram bure kabisa kwa muda ambao kifurushi chako kitakuwepo, yaani kama ulinunua kifurushi cha Masaa 24 WhatsApp, Facebook na Instagram zitakuwa bure kwa muda huo hata kama Dakika na MB zako zimekusha. Kama uko Dar es salaam unaweza kupata kifurushi hichi kwa kubofya *149*03#
Tigo Tanzania
Kwa upande wa Tigo vifurushi vingi vilivyopo ni vilevile vinavyopatikana kwenye menu ya kawaida ya *147*00# lakini pia kama unataka vifurushi vya muda wa maongezi unaweza kufuata hatua zifuatazo.
Andika SAA kupitia ukurasa wako wa SMS, Kisha tuma neno hilo kwenda namba 15509 kwa kufanya hatua hizi utaweza kupata muda wa lisaa limoja kuongea kwa gharama ya Tsh 100. Baada ya muda huu kuisha muda huo utaisha na ukiangalia kwa siku utakuta umetumia Tsh 2400.
Vilevile unaweza kupata vifurushi vingine kwa kupiga namba *148*03# au 148*02#
TTCL Tanzania
Kwa upande wa mtandao wa simu wa TTCL unaweza kupata bando la bei nafuu kwa kupitia menu ya *148*30# kisha chagua bandika bandua hapo utapata vifurushi vya internet nafuu zaidi. Unaweza kupata kuanzia MB 700 kwa siku kwa Tsh 500 na pia unaweza kupata hadi GB 8 kwa Tsh 5000, GB 3 utazitumia mchana hadi saa mbili usiku na GB 5 utazitumia kuanzia saa mbili usiku hadi saa 12 Asubuhi.
Halotel Tanzania
Kwa upande wa Halotel vifurushi vya bei nafuu zaidi vipo kwenye menu ya Vifurushi vya chuo ambavyo hivi ni lazima kupata laini ya Chuo. Unaweza kupata laini hii kwa mawakala wanaopita barabarani na hakikisha laini yako ni ya Chuo kabla ya kumpa hela. Ukishapata laini utapiga namba *148*55# alafu utaweza kupata vifurushi vya bei nafuu vya muda wa maongezi, SMS pamoja na Internet.
Airtel Tanzania
Kwa upande wa Airtel Tanzania unaweza kupata vifurushi vya bei nafuu kwa kubofya menu ya *149*99*03# na utapata vifurushi vya muda wa maongezi vya bei rahisi. Vilevile unaweza kupata vifurushi vya bei nafuu vya internet na muda wa maongezi pamoja na SMS kwa kubofya menu ya *149*99# kisha utaweza kuchagua UNI Ofa na hapo unaweza kupata vifurushi vya hadi kuanzia Tsh 500.
MUDA – Masaa 24 (Kwa Siku)
Airtel kwenda Airtel – Dakika 50
Mitandao Yote – Dakika 10
SMS – 1000
Internet – MB500
Bei – Tsh 500
MUDA – Kwa Siku 3
Airtel kwenda Airtel – Dakika 100
Mitandao Yote – Dakika 10
SMS – 1000
Internet – GB 1
Bei – Tsh 1000
MUDA – Siku 7
Airtel kwenda Airtel – Dakika 145
Mitandao Yote – Dakika 5
SMS – 1000
Internet – MB 750
Bei – Tsh 1500
Na hivyo ndio baadhi tu ya vifurushi ambavyo unaweza kupata kwa bei nafuu, kama kuna vifurushi vingine Tuwasiliane kupitia Whatsapp +255678714261