EPISODE YA 1:PADRE MLA NYAMA ZA WATU

On Kwa kuanza kujisimulia, Padri Moses anakataa katakata kutaja ni Padri wa madhehebu gani ya dini, kwani Anglikana na Romani wanatumia kofia hiyo ya upadri.
“Nimeshasema kuwa, naziba ili jamii inayonizunguka isielewe kitu chochote kutoka kwangu na siri hii ya aibu,” ndivyo alivyoanza kusimulia Padri Moses ‘Faza Moze’.
Anaendelea:
“Ilikuwa mwaka 1999, mwezi Desemba wakati wakristo wanajiandaa kwa sherehe ya Krismasi, kanisani walikuja wazee wawili ambao ni wageni machoni pangu miongoni mwa waumini wa kanisa langu hilo.
Walikaa fomu moja na waumini wengine, lakini katika kukaa walitenganishwa na mzee mmoja. Nikiwa naendelea na ibada, kila wakati niliwaona wale wazee wageni wakiangaliana kwa kupitia mgongoni kwa yule mzee aliyewatenganisha.
Kwa sababu moyo wangu ulikosa amani na wao, nikawa nawakazia macho hatua kwa hatua ili nione kila walichokuwa wakikifanya.
Kuna wakati nilishtuka sana kuona mmoja wao akibadilika sura na kuwa kama ya bundi, lakini nilipojiweka sawa kushangaa, akarudi katika sura ya kawaida, na mwenzake akacheka kama vile alijua mwenzake amegeuka sura na mimi nimeogopa.
Ndipo nilipoanza kukumbuka ujaji wao kama ulifanana na mazingira ya kuwa waumini wangu. Nikakumbuka kuwa, wakati wanaingia, walipitia njia zote za uumini, na pia walionekana ni wanyenyekevu kupita hata waumini wangu wa kila siku.
Wakati nikiwaza hayo, ghafla mmoja wa wale wazee alisimama mbele yangu bila kumwona akitoka kwenye fomu kuja mbele, nikashituka, lakini kumbe waumini wengine waliniona nilivyoshituka, wakakaza macho kwangu wakishangaa.
Nilikatisha maneno ya ibada na kuinua mikono juu kisha nikafanya ishara ya msalaba, kwa jina la baba, la mwana na la roho…
Akapotea mbele ya macho yangu na kuonekana amekaa na mwezake kama mwanzoni, wakacheka sana lakini si kwa kutoa sauti.
Kufuatia tukio hilo ambalo lilikuwa geni, niliendelea kuwaangalia wazee hao bila kusema kitu chochote.
Mmoja wa wazee hao aliponiona nimewakazia macho, alininyoshea kidole cha shahadu nikapoteza uwezo wa kuona.
Nikiwa katika hali hiyo, nilihisi kama kuna mtu amenigusa juu ya bega langu la kushoto ndipo nilinyosha mkono wangu ili nimguse.
Baada ya kufanya hivyo, nilifumbuka macho lakini jambo la kushangaza sikumuona mtu huyo na nilipoangalia mbele walikokaa waumini, niliwaona wale wazee wawili wakicheka huku wakiniangalia.

Endelea

Post a Comment

0 Comments